mobile header
10 March 2019 Viongozi kutoka kote duniani wakusanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ili kubuni ufumbuzi wa uchumi endelevu

Zaidi ya watu 4,700 wamekusanyika ili kubuni sera mpya, teknolojia na ufumbuzi bunifu wa kutimiza matumizi na uzalishaji endelevu. Matokeo kutoka kwa mkutano huu...

Press release
  • Zaidi ya watu 4,700 wamekusanyika ili kubuni sera mpya, teknolojia na ufumbuzi bunifu wa kutimiza matumizi na uzalishaji endelevu.
  • Matokeo kutoka kwa mkutano huu yatatumika kuweka ajenda ya kimataifa kuhusu mazingira na kuboresha uwezekano wa kufaulu kwa Mkataba wa Paris na Ajenda ya 2030.
  • Sayansi mpya kuhusu hali ya mazingira na suluhisho za changamoto zinazotukumba zitazinduliwa katika mkutano.

Nairobi, tarehe 10 Machi 2019 – Zaidi ya marais, mawaziri, viongozi wa biashara, maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa vyama vya kiraia wapatao 4,700 watakusanyika mjini Nairobi katika mkutano wa makao makuu ya mazingira duniani, ambapo watafanya maamuzi ambayo yataziwezesha jumuiya za kimataifa kufuata mitindo endelevu zaidi.

Mkutano wa nne wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa utafanyika kutoka tarehe 11-15 Machi chini ya mada ya Ufumbuzi Bunifu wa Kukabiliana na Changamoto za Mazingira, na Matumizi na Uzalishaji Endelevu.

Huu ndio mkutano mkubwa zaidi katika historia fupi ya Baraza hili, na mahudhurio yake ni karibu mara mbili kuliko mkutano wa mwisho uliofanyika Desemba 2017. Viongozi wakuu kutoka kote duniani watahudhuria, ikiwa ni pamoja na Marais wa Ufaransa na Kenya, Emmanuel Macron na Uhuru Kenyatta, na Wakurugenzi Watendaji wa mashirika makuu.

 

Maamuzi na matokeo madhubuti yanatarajiwa kuzalishwa huku wajumbe wakijadilina hadi usiku wa manane kwa siku tano. Maazimio yamependekezwa ili kushinikiza zaidi ili kuwezesha kufuata mitindo endelevu ya matumizi na uzalishaji, kuahidi kulinda mazingira ya baharini dhidi ya uchafuzi wa plastiki, kupunguza uharibifu wa chakula, na kuboresha ubunifu wa teknolojia wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kupunguza matumizi ya rasilimali na uharibifu wa viumbe hai.

 

Kwamba Baraza hili ndilo shirika la pekee la Umoja wa Mataifa nje ya Baraza Kuu ambapo mataifa yote wanachama hukutana, na uwezo wake wa kuunganisha sekta zote, inamaanisha kuwa ajenda ya mazingira ya kimataifa huitafafanuliwa hapa. Maamuzi yake yataathiri sana malengo ya Mkataba wa Paris na Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, pamoja na kuwezesha Mkutano wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa ya Umoja wa Mataifa ya 2019 na kuathiri ajenda ya Umoja wa Mataifa.

 

Kabla ya mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mataifa, Joyce Msuya, aliyahimiza mataifa kuchukua hatua na kuanza kufanya mabadiliko halisi.

 

"Muda unakwisha. Hakuna wakati wa kutoa ahadi na kupiga siasa tu. Hakuna wakati wa kutoa ahadi tu na kuwa na uwajibikaji mdogo. Kilicho hatarini ni maisha na jamii, kama wengi wetu tunavyoijua na kuifurahia leo, "aliandika katika barua ya sera.

 

Wajumbe wanapokuja mjini Nairobi kuhudhuria Mkutano huu, idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa inahuzunishwa sana na habari za ajali ya ndege ya shirika la Ethiopian Airlines. Tunawatumia sala na ramberambe zetu familia za walioathirika. Tunafuatilia kwa karibu uchunguzi na matokeo ya ajali hii.

Ripoti ya uchunguzi wa idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa ya Baraza hili, inayotumika kama msingi wa kufasili matatizo na kupangia sehemu za kuchukuliwa hatua, inathibitisha umuhimu wa kuchukua hatua za dharura. Ripoti hii inakadiria kuwa thamani ya huduma za kimazingira kati ya mwaka 1995 na 2011 ilikuwa trilioni $4 hadi trilioni $20; inaonyesha jinsi shughuli za kilimo zinaendelea kuharibu mazingira, kwa gharama ya trilioni $3 kila mwaka, na kukadiria kuwa gharama zinazohusiana na uchafuzi ni trilioni $4.6 kwa mwaka.

"Zaid ya yote, wakati wa kutenda ni sasa," alisema Rais wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Waziri wa Mazingira wa Estonia, Siim Kiisler. "Tunajua tunaweza kujenga jamii endelevu zaidi, zenye mafanikio zaidi na jumuishi kwa kuhakikisha matumizi endelevu na uzalishaji ambao unashughulikia changamoto zetu za mazingira na usiombagua mtu yeyote. Lakini tutahitaji kudumisha hali mwafaka za kuwezesha hali hii. Na tutahitaji kutumia mbinu tofauti za kufanya mambo. "

 

Baraza hili pia litashuhudia uchunguzi mpya utakaozinduliwa na idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na toleo jipya la ripoti pekee kote duniani inayotoa maelezo ya kina kuhusu mazingira: Global Environment Outlook 6, iliyoandaliwa na wanasayansi na wataalamu 252 kutoka nchi zaidi ya 70. Wakati huo huo, Global Resources Outlook inayoandaliwa na Jopo la Rasilimali za Kimataifa, huchunguza uchimbaji wa nyenzo, ikiwa ni pamoja na mtazamo wa baadaye na mapendekezo ya jinsi ya kutumia rasilimali asili kwa njia endelevu zaidi.

"Ni dhahiri kwamba tunahitaji kubadilisha jinsi uchumi wetu unavyofanya kazi, na jinsi tunavyothamini vitu tunavyotumia," alisema Msuya. "Lengo lake ni kuvunja kuondoa uhusiano kati ya ustawi na ongezeko la matumizi ya rasilimali, na kumaliza utamaduni wetu wa utupaji taka."

 

Baraza hili halihusu tu maazimio na sayansi. Matukio ya ziada pamoja na maonyesho yanawapa washiriki fursa ya kuanzisha ushirikiano na kutia saini mikataba inayowafaidi watu na mazingira.

 

Maonyesho ya Ubunifu Endelevu yanatumika kama kitovu cha uvumbuzi, huku teknolojia za mazingira na bidhaa za ubunifu zaidi ya 40 zikionyeshwa.

 

Mkutano wa One Planet Summit - ulioandaliwa kwa ushirikiano wa serikali za Ufaransa na Kenya, na Benki ya Dunia - pia unafanyika sambamba na Baraza hili, ukizingatia changamoto za mazingira ya Afrika.

Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Sera ya Biashara na Sayansi, lililoandaliwa kabla ya Baraza la idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa, lilizindua mipango yake kwa kutumia biashara mpya za kiasi kikubwa cha data na teknolojia zinazolinda mazingira ili kusuluhisha matatizo makubwa ya kimazingira.

 

KIDOKEZO KWA WAHARIRI

  • Ili upate maelezo zaidi, tembelea tovuti ya idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa
  • Pakua hamasisho la Mkurugenzi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa kwa Mataifa Wanachama.
  • Jiunge na mjadala kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia #SolveDifferent na utueleze hatua unazochukua ili kuhakikisha maisha endelevu kwa mstakabali wa sayari yetu.
Recent Stories
Story

Je, wajua kuwa unapotiririsha filamu mtandaoni, au unapotafuta jibu la swali fulani, unaathiri mazingira?…

Press release

Takriban watu 2,000  – wakiwemo watu wenye vyeo vya juu kutoka IBM, Google na Barclays – wanahudhuria Kikao cha Pili cha Dunia cha Kongamano…