mobile header
9 March 2019 UN inaongoza msukumo mpya wa pamoja wa uvumbuzi wa teknolojia zinazolinda mazingira

Takriban watu 2,000  – wakiwemo watu wenye vyeo vya juu kutoka IBM, Google na Barclays – wanahudhuria Kikao cha Pili cha Dunia cha Kongamano la Sera ya Biashara ya Umoja wa Mataifa Kongamano hili linazindua…

Press release
  • Takriban watu 2,000  – wakiwemo watu wenye vyeo vya juu kutoka IBM, Google na Barclays – wanahudhuria Kikao cha Pili cha Dunia cha Kongamano la Sera ya Biashara ya Umoja wa Mataifa
  • Kongamano hili linazindua mikakati ya kutumia data kubwa, masomo ya kimtambo, na biashara mpya ya teknolojia zinazolinda mazingira, kusuluhisha matatizo ya kimazingira, kibiashara na kijamii 
  • Kongamano hili pia linazindua mradi wa kuwa na miji na mifumo ya chakula endelevu na uongozi wa sekta za kibinafsi kuhusu mabadiliko ya hali ya anga

 

Tarehe 09 March 2019 – Mabingwa wa teknolojia, katika Umoja wa Mataifa,na jamii za sera, fedha na sayansi waliungana kuzindua misukumo mipya kuu kuhusu kutumia teknolojia muhimu kuunda suluhu safi, zinazolinda mazingira na faafu zaidi ili kufikia maendeleo endelevu.

Wakuu kutoka sekta hizi wanaungana na wawakilishi wa chama cha kiraia Jijini Nairobi katika Kikao cha Nne cha Mazingira ya Umoja wa Mataifa.

Lengo la Kongamano hili ni kuunganisha mashirika maarufu na watu kutoka sekta mbalimbali katika lengo moja la kutumia mazingira kwa uendelevu kwa manufaa ya kila mmoja. Mwaka huu, Kongamano hili linashuhudia uzinduzi wa mikakati miwili mikuu: Kundi la kwanza Linaloshughulikia Data Kubwa na Kuunganisha Akili isiyo Asilia na Kituo cha Biashara mpya ya Teknolojia Inayolinda Mazingira.

“Ni dhahiri kuwa kukua kwa teknolojia kwa kasi kulichangia pakubwa katika matatizo tunayokumbana nayo,” alisema Joyce Msuya, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mazingira ya Umoja wa Mataifa. “Lakini ni teknolojia hii hii – kupitia kwa uwezo wa binadamu wa kuvumbua na kubuni – ndiyo inayoweza kutuokoa. Mapinduzi ya Nne ya Viwanda inatoa fursa wazi ya kuunda suluhu safi zaidi, zinazolinda mazingira na faafu zaidi kufikia maendeleo endelevu.”

Kundi linaloshughulikia suala hili linalenga kujenga jukwa chanzo huria la data kubwa katika mazingira, na kugundua nafasi mpya katika Akili Isiyo Asili na masomo ya kimtambo. Inaunganisha mabingwa wa teknolojia, Mashirika ya Kuchunguza Ardhi, jamii za sayansi na sera, biashara mpya za teknolojia zinazolinda mazingira, wanasayansi raia na ulimwengu wa fedha na viwanda.

“Hatuwezi kuhakikisha utekelezaji wa Agenda ya 2030 pasipo data madhubuti, inayotuwezesha kutambua fursa, kuhakikisha tumefanya uamuzi unaotegemea ithibati, uwekezaji wa moja kwa moja na ufuatilizi wa hatua,” alisema Siim Kiisler, Rais wa Baraza hili na Waziri wa Mazingira wa Nchi ya Estonia. “Nina uhakika kuwa tutafanya maendeleo makubwa.”

Kwa sasa Kituo cha Biashara za Teknolojia zinazolinda Mazingira, kitatumika kama kiongeza kasi na kiangulia cha ubunifu mpya wa mazingira, kinapochunguza sera na hatua zinazohitajika ili kutumia ubunifu huu kubadilisha ulimwengu kuwa na mazingira bora na kuwezesha maisha endelevu.

Biashara mpya hazibadilishi tu masoko na maendeleo kibiashara, zingine zinasaidia kuokoa sayari hii. Uwekezaji wa Mtaji katika biashara mpya umeongezeka na kufikia upeo wa juu zaidi wa – bilioni $148 mwaka jana pekee. Zaidi ya kampuni 40-Zinazotegemea Mtaji Kubwa zimefikia thamani ya dolla -bilioni

Sehemu nyingine mpya ya kushughulikiwa katika Kongamano zitashughulikia miji na mifumo ya chakula endelevu na uongozi wa kibinfasi katika mabadiliko ya hali ya anga. Suluhu muhimu za kuzingatiwa zinajumuisha kutumia magari  yanayotumia umeme na mitindo mipya ya majengo yanayolinda mazingira, yanayoweza kuboresha matumizi ya rasilimali asilia kwa ufaafu na kuhimiza chaguo za kubasra za kimazingira. Teknolojia hizi ni muhimu sana kwa maisha ya baadaye ya sayari yetu, tukikumbuka kwamba takriban asilimia 70 ya idadi ya watu wataishi katika miji kufikia mwaka wa 2050.

VIDOKEZO KWA WAHARIRI

Kuhusu Mazingira ya Umoja wa Mataifa

Mazingira ya Umoja wa Mataifa inaongoza katika kulinda mazingira ulimwenguni kote. Inatoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kwa kuchochea, kueleimisha na kuwezesha mataifa na watu kuboresha maisha bila kuharibu maisha ya vizazi vijazo. Mazingira ya Umoja wa Mataifa inafanya kazi pamoja na serikali, sekta za kibinafsi , chama cha kirai na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na ya Kimataifa kote ulimwenguni. 

Kuhusu Kongamano la Biashara la Sera ya Kisayansi.

Baada ya kuzinduliwa rasmi katika Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa Disemba 2017, Kongamano la Biashara la Sera ya Kisayansi la Umoja wa Mataifa linalenga kutambua na kuendeleza fursa za uwekezaji katika biashara zinazolinda mazingira zinazoendeshwa na: maendeleo katika sayansi na teknolojia, kuwezesha sera na ufadhili katika ubunifu. Kongamano hili, ambalo linajifadhili kikamilifu, lina zaidi ya taasisi 2000 husika –  zinazowakilisha ulimwengu wa biashara, sayansi na sera – na kuwapa washikadau fursa za kuonesha suluhu za biashara zilizotathminiwa zinazolinda mazingira. Linatumika pia kama kichocheo cha ushirikiano kwa kuleta pamoja utaalamu na maarifa ya jamii mbalimbali ili kuangua na kuharakisha hatua za kufikia maisha endelevu ya baadaye.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Shereen Zorba, Mkuu wa Science-Policy Interface and Knowledge Networks, [email protected], +254 788 526000,  
Recent Stories
Story

Je, wajua kuwa unapotiririsha filamu mtandaoni, au unapotafuta jibu la swali fulani, unaathiri mazingira?…

Press release

Zaidi ya watu 4,700 wamekusanyika ili kubuni sera mpya, teknolojia na ufumbuzi bunifu wa kutimiza matumizi na uzalishaji endelevu. Matokeo kutoka…