mobile header
4 March 2019 Tunawakaribisha mabingwa wetu saba vijana mjini Nairobi

Tunafurahia kuwakaribisha Young Champions of the Earth wa 2018 kwa Mkutano wa Nne wa Mazingira ya Umoja wa Mataifa. Washindi saba wa tuzo, waliofadhiliwa na…

Story

Tunafurahia kuwakaribisha nchini Kenya Young Champions of the Earth  kwa Mkutano wa Nne wa Mazingira ya Umoja wa Mataifa. Washindi saba wa tuzo, waliofadhiliwa na Covestro, wataungana na wajumbe wengine Jijini Nairobi kuanzia tarehe 11 hadi 15 Mwezi wa Machi 2019, kwa msururu wa mikutano na Matukio ya ngazi ya juu.

Tuzo la Young Champions of the Earth hutolewa mara moja kila mwaka kwa wanaochangia mabadiliko maalum wenye umri wa kati ya miaka 18 na 30 kwa ubunifu wao wa kipekee za kukabiliana na changamoto kuu duniani.

Washindi, wanaochaguliwa kutoka kila eneo duniani, hupokea uthamini, mafunzo ya kiwango cha juu, na ushauri maalum kuwawezesha kufumbua uwezo wa miradi yao ya ubunifu. Wote wanafanya kazi ili #SolveDifferent majanga ya mazingira.

Washindi wa shindano la mwaka jana wanashughulikia masuala mbalimbali. Heba Al-Farra, mshindi wa Asia Mashariki, ndiye mwanzilishi wa shirika la Women in Energy & Environment, shirika linaloendeshwa na wanachama ambalo linawawezesha na kuwasaidia wanawake katika sekta za kawi na mazingira katika Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini.

Katika Marekani Kaskazini, Miranda Wang na kampuni ya BioCellection wanaangazia tatizo la uchafuzi wa mazingira kupitia plastiki kwa kuzingatia utengenezaji upya plastiki ambazo hazijachakatwa, kuigeuza kuwa kemikali zisizo na athari kwa  vifaa vyenye thamani kubwa.

image

GATOR HALPERN, HUGH WELDON NA SHADY RABAB KATIKA HAFLA YA KUTUZA  YOUNG CHAMPIONS OF THE EARTH MJINI NEW YORK MWAKA 2018. PICHA IMEPIGWA NA SHIRIKA LA MAZINGIRA YA UMOJA WA MATAIFA

 

Kampuni ya Gator Halpern, inayojulikana kama Coral Vita inafanya kazi ya kulinda matumbawe muhimu—ambayo yanadidimia kwa kasi mno—kwa kuunda muungano ulimwenguni wa uvumbuzi wa kampuni ya  matumbawe ardhini. Gator ndiye bingwa wa Young Champion mwaka wa 2018 wa Amerika Kusini na nchi za Karibea.

Katika juhudi nyingine ya kulinda ekolojia ya bahari, Miao Wang alianzinsha founded Better Blue, ambao ni mfumo wa kuunganisha na kutathmini ekolojia unaomruhusu kila mpiga mbizi na kituo cha kupiga mbizi kote ulimwenguni kuwa watetezi wa kulinda bahari.

Miao ni mmoja wa mabingwa wawili wa Young Champions kutoka eneo la Eshia-Pacsifiki, pamoja na Arpit Dhupar, ambayo kampuni yake ya Chakr Innovation inakabiliana na uchafuzi wa hewa ikitumia mbinu bunifu kupunguza uchafuzi wa hewa kutoka kwa jenereta zinazotumia dizeli. Kaboni inayonaswa katika mchakato huu inatumika kuunda wino usioathiri mazingira.

Barani Uropa, Hugh Weldon alishiriki katika kuvumbua Evocco, ambayo ni programu ya simumahiri inayowaeleimisha watumiaji kuhusu wanavyoathiri mazingira kutokana na nunuzi wao wa chakula ili wasawazishe tabia yao ya ununuzi na nidhamu.

Na kutoka Afrika, Bingwa Mchanga Shady Rabab anajenga Rabab Luxor Art Collective, ambayo inawawezesha watoto kutumia plastiki kwa ubunifu kwa kuitumia kuunda ala za muziki.

Shughuli zao zitaanza kwa kuwa na mapumziko ya siku mbili katika Ziwa Naivasha kuanzia saa 9 hadi 10 Machi. Warsha huu maalum utakuwa na masimulizi, kuwasiliana na hadhira tofauti tofauti, kuchora hatua kubwa muhimu ya maendeleo na ushauri kuhusu kubadili tabia.

Katika wiki nzima ya Mkutano huu wa Kimazingira, wenye mada: ‘Suluhu Bunifu kwa changamoto za kimazingira na uzalishaji na matumizi endelevu,’ kila mmoja wa Mabingwa hawa atazungumza katika matukio ya ngazi ya juu na kuhudhuria vipindi vya utangamano pamoja na wajumbe kutoka kote ulimwenguni.

 

image
Hafla ya Washindi wa Young Champions of the Earth mjini New York, 2018. Picha imepigwa na idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa

Jumatatu, tarehe 11 Machi, Hugh atanena katika Tukio la Kwanza la Jopo la Maonyesho ya Uvumbuzi Endelevu ya 2019 kuhusu Kustawisha Data Kubwa katika Mazingira kwa Maendeleo Endelevu. Kipindi hiki kinalenga kuhusisha majadiliano kuhusu kustawisha data kubwa na akili isyo ya asili kwa mazingira.

Washindi watatu wa kike watahudhuria kipindi cha Kifungua Kinywa cha Mawaziri na Viongozi Wanawake itakayofanyika siku ya Jumatano, tarehe 13 Machi. Washiriki katika mkutano huu wa Kifungua Kinywa watajadili masuala ya jinsia, utumiaji na uzalishaji endelevu na ufanisi wa Malengo Endelevu ya Ukuaji.

Arpit na Miranda watazungumzia hadhira ya Alliance for High Ambition on Chemicals and Waste—kundi la viongozi wa mawaziri na wawakilishi wakuu wanaojitolea kutoka mashirika ya serikali mbalimbali, kiwanda na vyama vya kijamii, ili kuhimiza hatua katika viwango vingi kuhusu masuala yanayohusu kemikali na uchafu.

Wasaba hawa pia watakuwa na kipindi ambacho wote watazungumza yenye mada: "Uongozi kwa Vijana," ambapo wataongoza majadiliano yanayowalenga viongozi wa duniani ili kuwahusisha vijana katika mjadala wa mazingira.

 Tunatazamia wiki ya matukio muhimu na ya kukisimua hapa Kenya—Karibuni! Fuatilia tukio hili kisha ufuate kampeni ya #SolveDifferent kupata taarifa.

 

Ungependa kuwa Young Champion of the Earth in 2019? Tunamhimiza yeyote anayetaka kusababisha mabadiliko katika sayari yetu kutuma ombi la tuzo la Young Champion of the Earth, linalofadhiliwa na Covestro. Tuma ombi leo! Tovuti imefunguliwa kufikia tare 31 Machi.

Recent Stories
Story

Je, wajua kuwa unapotiririsha filamu mtandaoni, au unapotafuta jibu la swali fulani, unaathiri mazingira?…

Press release

Zaidi ya watu 4,700 wamekusanyika ili kubuni sera mpya, teknolojia na ufumbuzi bunifu wa kutimiza matumizi na uzalishaji endelevu. Matokeo kutoka…