mobile header
Kuhusu #SolveDifferent

"Hatuwezi kusuluhisha matatizo yetu kwa kutumia dhana zile zile zilizoyasababisha"
-- Albert Einstein --

Kikao cha nne cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kitafanyika jijini Nairobi kutoka tarehe 11 hadi 15 Machi 2019 chini ya Kaulimbiu "Masuluhisho bunifu ya kukabiliana na changamoto za mazingira na matumizi na uzalishaji endelevu".

Licha ya maendeleo yaliyovuviwa na Malengo ya Kimataifa, kuna kikwazo kimoja kinachoyazuia yote: chaguo tunazofanya katika maisha yetu ya kila siku yanaendelea kuchochea tabia za matumizi na uzalishaji zinazozidi kukiuka uwezo wa dunia yetu.

Katika pilkapilka za Baraza hili, idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa inaongoza kampeni ya kimataifa ya #SolveDifferent. Kampeni hii itazingatia mbinu ya kuamsha hisia na kufahamishana kuhusu gharama ya mazingira ya miundo muhimu ya matumizi na uzalishaji.

Kuhusu Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa

Baraza la mazingira la Umoja wa Mataifa ni duniani taasisi ya juu zaidi duniani inayofanya maamuzi kuhusu mazingira. Baraza hili hushughulikia changamoto kuu za kimazingira zinazoikabili dunia ya leo. Kuelewa changamoto hizi na kuhifadhi na kukarabati mazingira yetu ndio uti wa Ajenda ya Mwaka 2030 kwa Maendeleo Endelevu.

Baraza la Mazingira huandaliwa mara mbili kwa mwaka kuweka vipaumbele vya sera za kimataifa za mazingira na kutunga sheria za mazingira za kimataifa. Kupitia maazimio yake na wito wa kuchukua hatua, Baraza hili hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano wa serikali za mataifa mbalimbali kuhusu masuala ya kimazingira. Mchakato wa kufanya maamuzi huhitaji ushirikiano mpana, na ndiyo sababu Baraza hili hutoa fursa kwa watu wote wasaidie kubuni masuluhisho kwa ajili ya afya ya dunia yetu.

Kikao cha nne cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kitafanyika jijini Nairobi kutoka tarehe 11 hadi 15 Machi 2019 chini ya Kaulimbiu "Masuluhisho bunifu ya kukabiliana na changamoto za mazingira na matumizi na uzalishaji endelevu".